Mali_ Waziri Mkuu wa Mali Chogeul Maiga amefutwa kazi
Mali: Waziri Mkuu wa Mali Choguel Maiga amefutwa kazi baada ya kukosoa serikali ya tawala kushindwa kuandaa uchaguzi ndani ya kipindi cha mpito cha miezi 24. Abedi Jean dela croix na undani zaidi.
Drc_ Mtu mmoja ameuliwa na wengine hawajulikane walipo baada ya shambulio la ADF
Drc: Mtu mmoja ameuawa na wengine hawajulikane walipo baada ya shambulio la ADF huko Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mwandishi wetu M’molelwa Mseke Dide ametuandalia ripoti ifuatayo kutoka Beni-Drc.
Drc_ Serkali ya Drc inashtumu waasi wa M23 kufanya mauaji ya kikabila
Waziri wa mambo ya ndani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jacquemain Shabani, anawashutumu waasi wa M23 kwa mauaji ya kikabila, na kuwasili kwa idadi kubwa ya raia wa kigeni katika maeneo ya Rutshuru na Masisi, Kivu Kaskazini nchini humo, ambako wenyeji walikimbia ghasia. Abedi Jean dela croix …
Uganda_ Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye amewekwa rumande
Mwanasiasa wa upinzani wa muda mrefu nchini Uganda Kizza Besigye, ameripotiwa kutekwa wakati akiwa nchini Kenya, ambapo kwa sasa anazuiliwa katika gereza la kijeshi jijini Kampala nchini Uganda. Abedi Jean dela croix alifanya mahojiano na mwandishi wetu Cassius Ochokombege kutoka Kampala-Uganda, A…
Tanzania_ Tanzania yaomboleza vifo vya walioangukiwa na ghorofa Dar es salaam
Vikosi vya uokoaji nchini Tanzania vimesema, vimefanikiwa kupata mawasiliano na watu ambao bado wamenasa siku moja baada ya jengo la ghorofa nne kuporomoka jijini Dar es Salaam. Mwandishi wetu Prosper Kwigize amefuatilia mkasa huo na kututumia ripoti ifuatayo kutoka Tanzania.
Senegal_ Chama cha Pastef cha rais aliye madarakani kimeshinda ubunge Senegal
Chama tawala cha Senegal cha Pastef kimeshinda katika uchaguzi wa wabunge ambao ulifanyika jana Jumapili. Abedi Jean dela croix na ripoti kamili.
Drc_ Wataalamu wa kijeshi wa Drc na Uganda wakutana Kinshasa nchini Drc
Drc: Wataalamu wa kijeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Uganda, wakutana katika mji mkuu wa Drc "kinshasa", kuratibu utekelezaji wa maagizo ya Tshisekedi na Museveni katika mapambano dhidi ya waasi wa ADF Mashariki mwa Drc. Nixon Katembo alifanya mahojiano na Omar Kavota, ambaye ni mchamb…
Sudan_ Teknolojia ya Ufaransa inatumiwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe Suda
Sudan: Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limesema teknolojia ya kijeshi ya Ufaransa inatumiwa katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan, na kukiuka vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa. Manasse bin Bendera na ripoti kamili.
Drc_ Ujumbe wa Monusco umefanya mkutano na wawakilishi wa wakaaji huko Beni-Drc
Drc: Ujumbe wa Monusco kutoka mjini Kinshasa unaendesha vikao na wawakilishi wa wakaaji jijini Beni; wakitaka washirikishwe kwenye operesheni Shujaa inayoshirikisha Nchi za Drc na Uganda. Mwandishi wetu M'molelwa Mseke Dide ametuandalia ripoti ifuatayo kutoka Beni-Drc.
Namibia_ Wanamibia wanaoishi nje ya nchi wamepiga kura hii leo kumchagua Rais
Namibia: Wanamibia wanaoishi nje ya nchi wamepiga kura wakati wa zoezi maalum la upigaji kura leo katika misheni ya kigeni ya Namibia. Manasse bin Bendera na ripoti kamili.