AFRIKA KUSINI - RAIS RAMAPHOSA ATANGAZA MASHARI MAPYA DHIDI YA CORONA
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alilihutubia taifa hiyo jana na kutangaza baadhi ya makataa, ili kuzuia kuenea kwa maambukizi ya virusi vya corona.
AFRIKA YA KATI - MSAFARA WA MSF WASHAMBULIWA
Shirika la madaktari bila mipaka limesema kuwa mwanamke mmoja ameuawa baada ya msafara shirika hilo kushambuliwa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.
BURUNDI - WATU 15 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA BASI
Watu 15 wameuawa katika shambuliz la basi nchini Burundi baada ya wetu wenye silaha kufunga barabara kufiatulia risasi abiria waliokuwa wakisafiri kwenye mkoa wa Muramvya kuelekea mjini Bujumbura .
MJADALA - MABADILIKO YA SIASA ZA KENYA
Mapema wiki hii tume huru ya uchaguzi nchini Kenya, Ilisema kwamba ahiko tayari kuandaa uchaguzi mkuu nchini humo kama inavyotarajiwa na wakenya wengi. Mbali na hayo, Rais wa nchi hiyo anayemaliza mda wake madarakani Uhuru Kenyatta siku za hivi karibuni, alidai kumuunga mkono katika uchaguzi huo ki…
AFRIKA KUSINI - ACE MAGASHULE ASHITAKI CHAMA CHA ANC
Katibu Mkuu wa chama cha African National Congress ANC aliyesimamishwa wadhifa wake, Ace Magashule, amekipeleka chama hicho mahakamani kupinga kusimamishwa kwake baada ya kukataa kujiuzulu.
ETHIOPIA - ZAIDI YA WATU HAMSINI WAUAWA TIGRAY
Zaidi ya watu 50 wakiwemo raia, wameuawa katika mashambulio ya angani yanayosemekana kutekelezwa na vikosi vya anga vya Ethiopia, katika soko moja karibu na mji mkuu wa Jimbo la Tigray, Mekelle
IVORY COAST - WAZIRI MKUU WA ZAMANI GUILLAUME SORO APEWA KIFUNGO CHA MAISHA
Waziri Mkuu wa zamani wa Ivory Coast Guillaume Soro ahukumiwa kifungo cha maisha. Waziri mkuu huyo wa zamani wa Ivory Coast alipatikana na hatia ya makosa ya uhaini na pia kuhatarisha usalama wake rais wan chi hiyo.Taarifa ya hukumu ya kifungo cha maisha jela dhidi ya Guillaume Soro ilitolewa wakat…
MOZAMBIQUE - MKUTANO WA KILELE WA VIONGOZI WA SADC MJINI MAPUTO
Viongozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika SADC, wanakutana leo hii mjini Maputo nchini Msumbiji, kujadili maswala mbalimbali likiwemo pia la maendeleo.
BURKINAFASO - WANAJESHI KUMI NA MMOJA WAUAWA NA MAGAIDI
Askari polisi 11 wameuawa na wengine wanne haijulikani walipo nchini Burkinafaso, baada ya shambulizi la kuvizia, wakati wakijielekeza kuchukuwa nafasi ya wenzao waliokuwa kwenye doria kaskazini mwa nchi hiyo.
NIGERIA - MAHAKAMA YA ECOWAS YAAMURU SERIKALI KUHUSU TWITTER
Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, imeiambia serkali ya Nigeria kwamba, iachane na mpango wake wa kukandamiza wa Nigeria kutumia mtandao wa kijamii wa Twitter, na kusema kuwa ni kinyume cha sheria.