Drc: Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku shughuli za chama cha PPRD cha rais wa zamani Joseph Kabila, pamoja na vyama vingine 12 vya kisiasa, nchini kote.
Uamuzi huo umetangazwa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Jacquemain Shabani, siku tatu tu baada ya Joseph Kabila kutangaza kuundwa kwa vuguvugu jipya la kisiasa na kijeshi linalojulikana kama FRN.
Ili kufahamu zaidi maana ya uamuzi huo na athari zake katika hali ya kisiasa nchini DRC, Abedi Jean Dela Croix amezungumza na Omar Kavota, mchambuzi wa siasa za Drc na eneo la Maziwa Makuu, na hii hapa sehemu ya mahojiano hayo.

Tanzania_ Mkutano wa mawaziri wa Afrika mashariki, kaskazini na kusini wafanyika
04:32

Kongamano la 26 la vyama vya ushirika vya akiba wafanyika Dar es salam
06:06

Ghana imewarejesha raia 120 wa Nigeria nchini mwao
04:58