News in KiSwahiliNews in KiSwahili

WAZIRI WA NISHATI ATANGAZA RUZUKU YA DOLA 43 MILIONI

View descriptionShare

Waziri wa Nishati, January Makamba amesema Jumanne Mei 10, Serikali imetoa ruzuku ya shilingi 100 bilioni sawa na dola 43 milioni ili kupunguza bei ya mafuta nchini.

Akizungumza Bungeni Bw Makamba alisema ruzuku hiyo itapunguza matumizi ya serikali kwa kipindi kilichosalia cha mwaka wa fedha 2021/22. Alisema ruzuku hiyo haitaathiri miradi ya maendeleo inayoendelea.

“Rais wetu, Samia Suluhu Hassan ameagiza mwaka ujao wa fedha ulikuwa mbali, hivyo itafutwe ahueni haraka. Kwa hiyo, kama hatua ya dharura, katika kipindi hiki kabla hatujafika mwaka mpya wa fedha, Serikali itatenga Sh100 bilioni ili kupunguza bei ya mafuta nchini.

“Ruzuku ya Sh100 bilioni itaanza kutumika kuanzia Juni 1, 2022. Hii inatokana na ukweli kwamba wauzaji wa jumla wameshalipa gharama za mafuta zilizojumuishwa katika bei ya Mei 2022 na tayari vituo vya mafuta vimenunua mafuta kwa bei ya sasa,” alisema Makamba. .

Siku ya Jumapili usiku Rais Samia Suluhu Hassan aliziagiza wizara na mamlaka zinazohusika kushughulikia mara moja kupandisha bei ya mafuta na kutafuta suluhu ya haraka.

Rais Samia Suluhu Hassan  aliyasema hayo katika kikao cha dharura kilichofanyika Ikulu Dar es Salaam majira ya saa kumi na mbili jioni Jumapili.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba na Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba.

Wengine ni Kamishna Mkuu wa idara ya forodha TRA, Alphayo Kidata na makatibu wakuu kutoka wizara za Fedha na Nishati.

Bei ya mafuta nchini Tanzania imevuka kiwango cha Sh3,000 kwa bidhaa zote tatu (petroli, dizeli na Mafuta ya Taa) katika miji ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara, kulingana na orodha ya bei ya hivi karibuni iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) .

  • Facebook
  • Twitter
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)