News in KiSwahiliNews in KiSwahili

WANAJESHI WANANE WAUAWA NA MAGAIDI KASKAZINI MWA TOGO

View descriptionShare

Wanajeshi wanane waliuawa na 13 kujeruhiwa katika shambulizi kaskazini mwa Togo siku ya Jumatano, serikali ilisema, ikiashiria uwezekano wa uvamizi wa kwanza wa mauaji katika taifa hilo na wanamgambo wa Kiislamu ambao wameua maelfu katika nchi jirani.

Kabla ya mapambazuko, kundi la watu wenye silaha kali walivamia kituo cha jeshi katika mkoa wa Kpendjal karibu na mpaka na Burkina Faso, serikali ilisema katika taarifa.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulio hilo. Serikali ililaumu "magaidi", bila kutoa maelezo zaidi.

Wachambuzi wa masuala ya usalama walisema shambulio hilo huenda lilitekelezwa na tawi la ndani la al Qaeda ambalo lina makao yake nchini Mali lakini katika miaka ya hivi karibuni limeenea kusini mwa Burkina Faso.

Makundi yenye uhusiano na Islamic State na al Qaeda yamefanya mamia ya mashambulizi katika ukanda wa Sahel huko Afrika Magharibi katika miaka ya hivi karibuni, yakilenga zaidi nchi zisizo na bandari za Burkina Faso, Niger na Mali.

Togo hadi sasa imeepushwa na ghasia hizo, ambazo zimewalazimisha mamilioni ya watu kukimbia makazi yao, lakini wataalam wa usalama wameonya kuhusu kuenea kwa operesheni ambazo zinaweza kuhusisha mataifa ya pwani kama Togo.

Mnamo mwaka wa 2018, jeshi la Togo lilianzisha operesheni ya kukomesha vikundi vya Kiislamu vinavyoingia kutoka kaskazini. Vikosi vya usalama vilizima shambulio la watu wenye silaha kwenye kambi moja katika eneo moja na shambulio la Jumatano mnamo Novemba 2021, bila kupata hasara. Serikali ilisema wakati huo kwamba washambuliaji walikuwa wamefika kwenye mpaka kutoka Burkina Faso.

Nchini jirani ya pwani ya Togo, Benin, imeshuhudia ongezeko kubwa la mashambulizi karibu na mpaka wake wa kaskazini na Burkina Faso. Wanajeshi watano waliuawa mwezi uliopita wakati msafara wa jeshi ulipogonga kilipuzi.

Washirika wa kimataifa wakiongozwa na Ufaransa wametumia mabilioni ya dola na kupeleka maelfu ya wanajeshi kudhibiti mashambulizi hayo yaliyoanza nchini Mali mwaka 2012 kabla ya kusambaa katika nchi za Niger na Burkina Faso.

Lakini hadi kufikia sasa ghasia zinaendelea, haswa katika maeneo duni ya vijijini ambapo vikundi vya wanajihadi wanaishi miongoni mwa raia.

Ukosefu huo wa usalama umedhoofisha hali ya demokrasia katika nchi ambazo wakaazi wamechoshwa na ghasia na kutafuta mabadiliko. Nchini Mali na Burkina Faso, wanajeshi wamenyakua mamlaka tangu 2020, na kuahidi kuimarisha usalama.

  • Facebook
  • Twitter
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)