News in KiSwahiliNews in KiSwahili

WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA URUSI AKUTANA NA RAIS WA ALGERIA

View descriptionShare

Waziri wa mambo ya nje wa Urusi alikutana  jana Jumanne na rais wa Algeria, kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili kwa matumaini ya kuimarisha  uhushirikiano wa mataifa hayo.

Waziri wa Mambo ya Nje Sergey Lavrov aliwasilisha mwaliko kutoka kwa Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kiongozi wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune, kuzuru Moscow, shirika rasmi la habari la APS la Algeria lilisema. 

Madhumuni yaliyotajwa ya ziara hiyo yatakuwa ni kuimarisha uhusiano wa nchi mbili katika nyanja zote, kutoka kwa kijeshi hadi kwa kibinadamu, APS iliripoti. Kwa muda mrefu Urusi imekuwa ikilipatia taifa hilo la Afrika Kaskazini vifaa vya kijeshi. Lavrov amesema kuwa “ushirikiano wa kijeshi na kiufundi,” na alionyesha kuridhika kwa Urusi na “imani iliyowekwa kwetu (na Algiers) katika eneo hili.”

Algeria nchi yenye utajiri wa gesi iko katika hali tete kuhusu uhusiano wake wa muda mrefu na Urusi. Katika siku za hivi karibuni baada ya kuibuka vita kati ya Urusi na Ukraine, sasa inazidi kutiliwa macho na nchi zinazotafuta kupunguza utegemezi wao wa nishati ya Kirusi. 

  • Facebook
  • X (Twitter)
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)