Shirika la Fedha Duniani (IMF) limesema huenda likasimamisha ushirikiano wake wa kifedha na serikali ya federali ya Somalia katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, iwapo nchi hiyo ya Pembe ya Afrika itaahirisha tena uchaguzi.
Hayo yalisemwa Jumanne na Laura Jaramillo Mayor, Mkuu wa ofisi ya IMF nchini Somalia na kuongeza kuwa, "Mipango ya IMF nchini Somalia itaangalia upya katikati ya Mei, lakini kuendelea kuakhirishwa uchaguzi kuna maana kwamba serikali mpya huenda isiweze kuidhinisha mageuzi mapya kwa wakati mwafaka."
Amesema iwapo IMF itachukua hatua ya kuisimamishia Somalia msaada, basi bajeti ya nchi hiyo maskini ya Kiafrika itaathiriwa pakubwa, na vile vile mpango wa kuipunguzia deni la taifa kutoka dola bilioni 5.2 za Marekani la kuanzia mwaka 2018, hadi dola milioni 557.
English:
IMF says Somalia funding at risk over election delays
The International Monetary Fund (IMF) could stop its programme in Somalia in three months if long-postponed national elections encounter new delays. The IMF’s programme in Somalia is due for a review in mid-May, but election delays mean that a new administration may not be ready to endorse planned reforms in time, Laura Jaramillo Mayor, the fund’s mission chief for the country, said on Tuesday.