News in KiSwahiliNews in KiSwahili

MALI: Bunge la Mali laidhinisha muda wa mpito  wa miaka mitano

View descriptionShare

Wabunge wa Mali siku ya Jumatatu waliidhinisha mpango unaoruhusu serikali ya kijeshi kutawala kwa  miaka mitano, licha ya vikwazo vya kikanda vilivyowekwa kwa nchi hiyo kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi.

Bunge linaloongozwa na jeshi pia liliamua kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo hawezi kugombea uchaguzi wa kidemokrasia ujao, kama sehemu ya mswada huo huo. Baada ya kufanya mapinduzi katika taifa hilo maskini la ukanda wa Sahel mnamo Agosti 2020, watawala wa kijeshi wa Mali waliahidi kuandaa uchaguzi mnamo Februari 2022.

Lakini mwezi Disemba mwaka jana, serikali ya kijeshi ilipendekeza kusalia madarakani kati ya miezi sita na miaka mitano, ikitaja masuala ya usalama. Hata hivyo kayika kujibu, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) mwezi uliopita iliweka vikwazo vya kibiashara na kufunga mipaka yake na Mali. ECOWAS imeitaja kuwa mud wa mpito  unaopendekezwa na serikali ya kijeshi  haukubaliki.

English:

Mali parliament approves five-year democratic transition plan

Mali’s lawmakers have approved a plan allowing the military government to rule for up to five years, AFP journalists said, despite regional sanctions imposed on the country over delayed elections. The army-dominated legislature also decided that the country’s interim president cannot stand for a future democratic election, as part of the same bill.

  • Facebook
  • X (Twitter)
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)