News in KiSwahiliNews in KiSwahili

ETHIOPA: Waziri Mkuu wa Ethiopia akanusha kuanzishwa mazungumzo na waasi wa TPLF

View descriptionShare

Waziri Mkuu wa Ethiopia Aby Ahmed anasema kuwa hakuna mazungumzo ambayo yameanza na chama cha wanaharakati wa ukombozi wa watu wa Tigray (TPLF) ili kumaliza mzozo kaskazini mwa nchi hiyo.  Tamko hili ni kinyume na madai ya kiongozi wa TPLF Debretsion Gebremichael wiki iliyopita kwamba mazungumzo yalikuwa yakiendelea na kwamba kuna matumaini ya kumaliza mgogoro huo kwa amani.

Katika hotuba yake ya kwanza bungeni tangu aapishwe kwa muhula mpya mwezi Oktoba, Abiy alisema: “Nasikia mengi kuhusu mazungumzo, lakini hakuna mazungumzo yoyote hadi sasa. Hata hivyo, kwa sababu tumesema hatujazungumza haimaanishi kwamba hakutakuwa na mazungumzo kabisa.”

Mapigano yalizuka katika eneo la kaskazini mwa Ethiopia la Tigray mnamo Novemba 2020, na wapiganaji wa TPLF walisonga mbele kuelekea mji mkuu, Addis Ababa, kabla ya kurudishwa nyuma na vikosi vya serikali na washirika. Tigray pia amekumbwa na mzozo mkubwa wa chakula na afya, huku msaada mdogo ukiingia katika eneo hilo.

English:

 No peace talk has commenced with TPLF: Ethiopia Prime Minister Aby Ahmed

Ethiopia’s Prime Minister Aby Ahmed says that no talks have commenced with the Tigray People’s Liberation Front (TPLF) to end the crisis in the north of the country. This declaration is contrary to TPLF leader Debretsion Gebremichael’s claim last week that talks were under way and that there was hope to end the crisis peacefully.

  • Facebook
  • X (Twitter)
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)