News in KiSwahiliNews in KiSwahili

BURKINA FASO: Mlipuko karibu na mgodi wa dhahabu waua watu 60 nchini Burkina Faso

View descriptionShare

Mlipuko mkubwa uliotokea karibu na mgodi wa dhahabu huko kusini magharibi mwa Burkina Faso umesababisha vifo vya watu 60 na kujeruhi wengine zaidi ya mia moja. Mlipuko huo umetokea katika ghala la mada za kemikali zinazotumiwa kusafishia madini ya dhahabu.

Sansan Kambou ambaye ni mlinzi wa mazingira aliyekuwepo eneo la tukio hilo amesema maiti nyingi za watu zilitapakaa huku na kule. Watu walioshuhudia wamesema milipuko kadhaa ilisikika kwa kufuatana katika eneo hilo.

Burkina Faso ina kasi kubwa ya uzalishaji wa madini ya dhahabu barani Afrika na kwa sasa inashika nafasi ya tano katika uzalisha wa madini hayo. Karibu watu milioni 1.5 wanafanya kazi katika sekta ya madini ya dhahabu nchini Burkina Faso na thamani na uzalishaji wa tasnia hiyo mwaka 2019 ilitangazwa kuwa ni karibu dola bilioni 2.

English:

Explosion reportedly kills 60 people near Burkina Faso gold mine

An explosion near a gold mining site in south-western Burkina Faso has killed 60 people and injured more than 100 others.  According to witnesses and the national broadcaster, the explosion, which happened on Monday, was believed to have been caused by chemicals used to treat gold stocked at the site

  • Facebook
  • X (Twitter)
  • WhatsApp
  • Email
  • Download

News in KiSwahili

A news and current affairs show produced live by the current affairs team.
Social links
Recent clips
Browse 1,121 clip(s)