MALI_ KUSITISHA MAZUNGUMZO MAPYA. 15_07_2022(1)Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Mali imekitaka kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini humo (MINUSMA), kusimamisha safari zote za ndege zilizopangwa kusafirisha askari wake, baada ya mamlaka ya nchi hiyo kuwazuilia wanajeshi 49 kutoka Ivory Coast, ambao waliingia katika ardhi yake kushiriki katika operesheni za usalama bila ya kupata vibali. Ripoti ya Manasse Bin Bendera na Mengi zaidi.